Mwanajeshi wa Marekani akamatwa na Mabomu Tanzania

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 weeks ago
rickmedia: mwanajeshi-marekani-akamatwa-mabomu-tanzania-678-rickmedia

 Jeshi la Polisi mkoani Tarime na Rorya limemkamata Charles Onkuri Ongeta (30), mwenye uraia wa Marekani na Kenya na ambaye ni Sajenti wa Jeshi la Marekani, akiwa na mabomu manne ya kurushwa kwa mkono aina ya CS M68.

Ailikamatwa Novemba 16, 2025 mida ya saa sita mchana katika mpaka wa Sirari akitokea Kenya kwa gari aina ya Toyota Landcruiser yenye namba KDP 502 Y.

Polisi wamesema hata kwa kibali, aina hiyo ya silaha hairuhusiwi kuingizwa nchini. Uchunguzi na uhojiwaji unaendelea kwa ajili ya hatua za kisheria.