Mzazi mwenzake na Elon Musk aishtaki AI Ya Elon Musk

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 hours ago
rickmedia: mzazi-mwenzake-elon-musk-aishtaki-elon-musk-927-rickmedia

Ashley St. Clair (27), mama wa mtoto wa bilionea Elon Musk, ameiwasilisha kesi katika Mahakama ya New York dhidi ya kampuni ya xAI inayomiliki akili mnemba ya Grok.

Anadai Grok ilizalisha na kusambaza picha bandia za kingono bila idhini yake. Katika mashtaka ya Januari 13, 2026, Ashley ameishutumu Grok kwa unyanyasaji wa kidijitali, ikiwemo kuvua nguo kwa njia ya teknolojia na kudhalilisha waathirika.

Kufuatia tuhuma hizo, xAI imethibitisha kuwa Grok haitahariri tena picha za watu halisi kwenye mtandao wa X. Ashley anasema maudhui hayo yaliendelea hata baada ya yeye kupinga hadharani.

Anadai pia yeye na Elon Musk waliwahi kuwa na uhusiano na wana mtoto wa kiume aliyezaliwa 2024.