Jair Bolsonaro, rais wa zamani wa Brazil, jana alianza kutumikia kifungo cha miaka 27 jela adhabu aliyopata akikabiliwa na mashitaka ya kuongoza jaribio la mapinduzi.
Uamuzi huo ulitolewa na Alexandre de Moraes, jaji wa Supreme Federal Court of Brazil, ambaye amemzuia Bolsonaro kuendelea na mashauri yoyote ya rufaa.
Bolsonaro amewekwa katika makao makuu ya polisi ya shirikisho huko Brasilia katika chumba cha m² 12, chenye kitanda, bafu ya kibinafsi, chumba cha hewa, televisheni na dawati. Hakutakuwako mawasiliano na wafungwa wengine wachache waliopo pale.