Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya amesema Lengo la kufanya hivyo ni ili kuwa na Sera ya Kodi inayotabirika na kuwafanya Wawekezaji kuweka mipango yenye ufanisi.
Ameeleza marekebisho yaliyofanyika Mwaka 2023 hayatafanyika tena hadi Miaka mitatu ili kuwa na Sera za Kodi inayotabirika.
Amesema “Awali Wananchi walisema bajeti ni ya pombe, Sigara na Soda, maana ya kauli hizo ni kuwa kila Mwaka Serikali ilikuwa inabadilisha Viwango vya Kodi vilivyokuwa vinatozwa kwenye Bidhaa hizo jambo ambalo kwa sasa halitakuwa linafanyika kila Mwaka.”