Watalii wakwama kwenye Mafuriko nchini Kenya

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: watalii-wakwama-kwenye-mafuriko-nchini-kenya-93-rickmedia

Takriban watalii 100 ni miongoni mwa mamia ya watu waliokwama baada ya mto kufurika katika hifadhi ya wanyamapori maarufu ya Maasai Mara nchini Kenya kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo hayo.

Ofisa mwandamizi katika Kaunti ndogo ya Narok Magharibi, Stephen Nakola ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba takriban watalii 100 au zaidi wamekwama katika nyumba za kulala wageni au kambi ya mbugani.

Hali ilivyo imesababisha pia ugumu wa kuzifikia baadhi ya kambi. Mbuga ya Maasai Mara iliyo kusini-magharibi mwa Kenya, ni kivutio cha watalii na makazi ya wanyamapori asilia wakiwemo wale wanaojulikana kama "Big Five", simba, tembo, vifaru, chui na nyati pamoja na twiga, viboko na duma.