Barcelona yanusa ubingwa, yaibamiza Real Madrid mara 4 mfululizo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

5 hours ago
rickmedia: barcelona-yanusa-ubingwa-yaibamiza-real-madrid-mara-mfululizo-796-rickmedia

Timu ya Barcelona imeifunga Real Madrid Magoli 4-3, ushindi unaoifanya ifikishe pointi 82 ikiwa na maana inahitaji alama 2 katika michezo mitatu iliyosalia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga), Madrid ikibaki nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 75.

Licha ya kupoteza Kylian Mbappé ameifungia Real Madrid magoli yote matatu (hat trick) na kushika nafasi ya kwanza ya Wafungaji wa LaLiga akifikisha magoli 27

Matokeo hayo yanaifanya Madrid kuwa imefungwa mara nne mfululizo msimu huu, michezo iliyopita; Barcelona 3-2 Real Madrid (Copa de Rey), Real Madrid 2-5 Barcelona (Super Cup) na Real Madrid 0-4 Barcelona (LaLiga).