Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jenerali Japhet Koome amewashutumu Wanasiasa kwa kukodi Maiti za Watu ambao walifariki kwa sababu mbalimbali iliwemo Magonjwa na Ajali kutoka Vyumba vya kuhifadhia Maiti na kudai ni waathiriwa wa Ukatili wa Polisi.
Katika Hotuba yake kwa Vyombo vya Habari, IGP Koome alisema baadhi ya Wanasiasa wanakula njama na Wahudumu wa 'Mochwari' ili kupiga picha za miili hiyo, na kisha kuziweka kwenye Mitandao ya Kijamii ili kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi.
Hivi karibuni Polisi Nchini humo wamekuwa wakishutumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa Maandamano ya Kupinga Serikali yanayoongozwa na Raila Odinga.