Nyundo na Wenzake Waomba Kesi Yao na Hukumu Kufutwa

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: nyundo-wenzake-waomba-kesi-yao-hukumu-kufutwa-642-rickmedia

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeendelea kusikiliza hoja za rufaa kupinga kifungo cha Maisha jela walichohukumiwa aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Clinton Damas, maarufu Nyundo na wenzake Amin Lema, Nickson Jackson na aliyekuwa Askari Magereza, Praygod Mushi, huku upande wa Jamhuri ukiomba kuzijibu Juni 12, 2025

Akiwasilisha hoja Mahakamani, Juni 10, 2025, Wakili wa Warufani hao, Godfrey Wasonga amedai kulikuwa na dosari za Kisheria katika kesi hiyo kuanzia hati ya mashtaka hadi hukumu. Amedai Mahakama ilioneshwa vipande Vinne vya Video ambavyo ni 6, 7, 8 na 9 lakini kwenye hukumu, vipande vya Video vilivyowatia hatiani ni namba 1, 2, 3 na 4 ambavyo havikuoneshwa Mahakamani hapo

Aidha, kwa mujibu wa Wakili huyo, vipande vya Video vilivyooneshwa viliwaonesha washtakiwa wakijirekodi wakiwa wanacheza Muziki, huku wakiwa na chupa za Vinywaji lakini hazikuonesha wakiwa wanatenda kosa la kubaka kwa kikundi wala kulawiti