Skales akana kusaidiwa na Burna Boy, Mashabiki wamshambulia

-rickmedia: Rick

Rick

5 months ago
rickmedia: skales-akana-kusaidiwa-burna-boy-mashabiki-wamshambulia-957-rickmedia

Baada ya kumuunga Mkono Rapa Speed Darlington ambaye hivi karibuni ameachia Diss Track kwa #BurnaBoy aliyoipa jina la #BabyOil mashabiki mbalimbali wameibuka na kumshambulia Skale kwa kitendo hicho kwa kumuita kuwa mtu asiyekuwa na shukrani kwa Burna Boy.

Kupitia Ukurasa wake wa 'X' Skales amewachana mashabiki kuwa hakuwahi kusaidiwa na Buran Boy ila kila mtu alinufaika kwenye kolabo yao waliowahi kuifanya. Skale amejimwagia maua yeye mwenyewe, Mungu na Mashabiki kumuweka kwenye ramani na si msaada wa mtu mwengine yeyote

"Nitajitetea siku zote, nampenda Burna Boy lakini msijaribu kusema kuwa alinisaidia. Hakuna aliyenisaidia ni mimi, Mungu na mpenzi ya mashabiki. Tulifanya kolabo vizuri na kila mtu alinufaika na ndio maana kila mtu anaitumia.

Skales na Burna Boy walikutana kwenye kolabo moja mwaka 2016 kupitia wimbo wa Skales "Temper"