Rais Samia apewa tuzo ya heshima na CAF

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

8 hours ago
rickmedia: rais-samia-apewa-tuzo-heshima-caf-584-rickmedia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Maalum na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kutambua mchango wake katika mchezo wa soka.

Tuzo hiyo imekabidhiwa Jumatano, Novemba 19, 2025 jijini Rabat, Morocco kunakofanyika hafla ya Tuzo za CAF 2025.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa serikali, Gerson Msigwa ndio amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Samia.