Timu ya Taifa ya Senegal imeshinda kombe la Shirikisho la Afrika (CAF) baada ya kumfunga Morocco kwa bao 1-0. Katika dakika za jioni Senegal waliingia ubaridi baada ya Morocco kupata penati kabla ya Braham Diaz kukosa.

Nyota wa mchezo kwenye mashindano haya amebeba mchezaji wa Timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane hii ni mara baada ya kuiongoza timu yake kushinda ubingwa.

Katika tukio litakalobaki kwenye historia ya Afrika ni tukio la wachezaji wa Senegal kususia mechi kwa kutoka uwanjani kwa kile walichoita upendeleo wa penati waliopewa Morocco. Akiwa kama kiongozi wa Timu Sadio Mane aliwaongoza wachezaji wenzake kurudi Uwanjani na baadae Idrissa Gueye akawainua Senegal kwa bao la ushindi na mchezo kuisha SENEGAL 1-0 MOROCCO.
Baada ya mchezo kutamatika Rais wa CAF Patrice Motsepe alimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo Paul Makonda Bendera ya CAF ikiashiria rasmi mashindano ya CAF msimu ujao yataandaliwa na Tanzania, Kenya na Uganda.