Eddy Kenzo Alalamika Diamond Kupendelewa Kushinda Wao

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

21 hours ago
rickmedia: eddy-kenzo-alalamika-diamond-kupendelewa-kushinda-wao-821-rickmedia

Staa wa Muziki kutoka Nchini Uganda #EddyKenzo amedai hajaridhishwa na Treatment aliyopewa Staa #DiamondPlatnumz Nchini Uganda kwenye Show ya #CoffeeMarathon lililofanyika hivi karibuni huko Ntungamo, ambapo #Diamond alipewa kile ambacho #Kenzo amekiita kama upendeleo wa wazi.

#Kenzo, ambaye hakuhudhuria mkutano na waandishi wa habari wa tukio hilo ambapo walikuwepo #BebeCool, #TheBen, #Truth256, na #DiamondPlatnumz, Alieleza masikitiko yake juu ya namna tukio hilo lilivyoendeshwa na waandaaji. Namna wasanii wa Uganda walivyotendewa ukilinganisha na #DiamondPlatnumz na kudai kuwa ilikuwa ni kuivua nguo tasnia ya muziki ya Uganda.

"Hauwezi kuniambia mmekodisha Ndege binafsi na Helkopa kwa ajili ya msanii Mgeni alafu Wasanii wa ndani hamuwafanyii hivyo hatuwezi kukaa kimya tukiona tunatendewa vitu vya hovyo.

#DiamondPlatnumz aliwasili Uganda kwa kutumia ndege binafsi ya kukodisha na kisha kutumia helikopta kufika kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Ntungamo kitu ambacho #EddyKenzo amedai ni kuwatenga wasanii wa Uganda.

“Sisemi haya kwa wivu,” aliongeza Kenzo. “Lakini sisi pia tunastahili kuwa kwenye jukwaa hilo na kufurahia upendeleo maalum, kwa sababu kama nisingekuwa wa thamani, musingenialika kwenye tukio hilo.”