Halle Bailey Akanusha Kuwa na Ugonjwa Wa Akili

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

13 hours ago
rickmedia: halle-bailey-akanusha-kuwa-ugonjwa-akili-468-rickmedia

 #HalleBailey amevunja ukimya na kukanusha madai yote ya #DDG kwamba historia yake ya kutishia kujidhuru inaweka hatarini ustawi wa mtoto wao.

Kulingana na #Billboard, alimweleza jaji kuwa msanii huyo wa rap anazidisha madai kuhusu matatizo yake ya afya ya akili ambayo tayari ameshayashughulikia, na kwamba yeye ni mzima asilimia 100 na ana uwezo kama mzazi wa mtoto wao.

#Bailey anaeleza kuwa matukio mengi ya matatizo ya afya ya akili yaliyonukuliwa na #DDG yalitokea mwaka wa 2022 na 2023 alipokuwa amevunjika moyo sana na tabia ya msanii huyo wa rap.

Hate hivyo, anasema DDG hakuwahi kueleza wasiwasi wowote kuhusu uwezo wake wa kuwa mzazi hadi siku ile madai yake ya unyanyasaji wa nyumbani yalipokuwa yamepangwa kusikilizwa mahakamani.