Aliyekuwa Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu afariki Dunia baada ya kuugu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

13 hours ago
rickmedia: aliyekuwa-rais-zambia-edgar-chagwa-lungu-afariki-dunia-baada-kuugu-449-rickmedia

Aliyekuwa Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa za kifo chake zimetolewa Alhamisi Juni 5, 2025 na chama chake cha zamani, Patriotic Front (PF), kilichothibitisha kuwa kiongozi huyo ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 68.

Lungu aliongoza Zambia kuanzia mwaka 2015 hadi 2021, baada ya kuchukua mikoba hiyo kutoka kwa Michael Sata ambaye ni marehemu hivi sasa.

Mwaka 2021, Lungu alishindwa katika uchaguzi mkuu na mpinzani wake wa muda mrefu, Hakainde Hichilema ambaye sasa ni Rais wa Zambia.