Waziri Mkuu wa Mongolia, Oyun-Erdene, amejiuzulu kufuatia maandamano makubwa yaliyozuka baada ya mtindo wa maisha ya kifahari wa mwanawe kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.
Mwanawe alionyesha begi la #Dior na mifuko kadhaa ya manunuzi alipokuwa kwenye likizo ya uchumba.
Picha ya begi la #Dior, inaripotiwa kupostiwa na mchumba wake, ilikuwa na maelezo yaliyosomeka: “Happy birthday to me” (Heri ya siku yangu ya kuzaliwa). Picha nyingine ilionyesha wanandoa hao wakibusiana wakiwa katika swimming pool.
Luvsannamsrain Oyun-Erdene, ambaye amekana kufanya kosa lolote, alipoteza kura ya imani bungeni siku ya Jumanne.