Jembe Ni Jembe Aanika Ukweli Kumsaidia Harmonize Pesa za Kumlipa Diamond

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

20 hours ago
rickmedia: jembe-jembe-aanika-ukweli-kumsaidia-harmonize-pesa-kumlipa-diamond-802-rickmedia

Mjasiriamali na moja ya viongozi wa lebo ya #KondeGang #JembeNiJembe Amefunguka kuhusu kumsaidia Staa wa Muziki #Harmonize kulipa madeni aliyokuwa akidaiwa na lebo yake ya zamani (WCB) Lakini pia pesa za kufungua lebo ya #KondeGang.

Akiwa kwenye kipindi cha #Centro cha #CloudsTv, #JembeNiJembe Amesema...

"Nikiwa kwenye harakati, nilikutana na #Harmonize aliniomba, alinieleza shida yake yote, changamoto alizokuwa nazo. Aliniambia ndoto zake niliona ni kijana mwenye kipaji ana ndoto na vision nzuri. Niliona nahitaji kumsaidia. Nilimsaidia Harmonize wakati akifungua record label yake. Alikuwa ana uhitaji wa fedha"

"Nilitoa fedha, nilimpatia ili aanzishe record label yake. Hata kulipa madeni aliyokuwa nayo katika record label yake iliyopita"

"Amefanikisha na nashukuru nimekuwa mmoja kati ya watu wanaochangia kukua kwa vipaji vya vijana hapa Tanzania"

Harmonize aliingia rasmi kwenye lebo ya WCB Wasafi (Wasafi Classic Baby) mnamo mwaka 2015, baada ya kupendwa na Diamond Platnumz kutokana na wimbo wake "Aiyola"

Baada ya miaka ya maendeleo na mafanikio, alitangaza rasmi kuondoka WCB mwishoni mwa mwaka 2019, na baadaye kuanzisha lebo yake mwenyewe, Konde Music Worldwide, mwezi wa Septemba 2019.