Pheelz amvuta Olamide kwenye EP yake ya "Triibe Tape"

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: pheelz-amvuta-olamide-kwenye-yake-triibe-tape-730-rickmedia

Nyota wa muziki kutoka Nigeria, ambaye pia ni mtayarishaji wa Muziki Pheelz, leo ametoa EP ya ya Pheelz Good( Triibe Tape) yenye nyimbo 4 ambazo kwa sasa zinapatikana kupitia Warner Records.

EP inangoma kama JOY' aliyomshirikishwa gwiji wa Afrobeats Olamide, kwa mujibu wa Pheelz anasema ‘’Joy’ ni wimbo maalum kwangu kwa sababu mimi na Olamide tumekuza udugu wetu na tumekuwa marafiki kwa miaka mingi".

Pia EP hiyo ina ngoma nyingine kama 'JELO' ambayo ilitoka muda kidogo na amemshirikisha Young Jonn, na pia kuna remix of “JELO” akimshirikisha Lekyz na Henry X, na ngoma nyinginr ni “Riddim & Blues.”

Akiongea leo amesema "Triibe Tape ni kazi nzuri ya Kabila na baada ya hapa, nitasafiri kote ulimwenguni kuungana na mashabiki. Kwa hivyo, ni mradi wa sisi kushirikiana nao kwenye jukwaa., na kuburudika na mziki mzuri".