Zuchu Aongeza Utambulisho na Sasa Anajiita Mrs Nasibu (Diamond Platnumz)

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: zuchu-aongeza-utambulisho-sasa-anajiita-mrs-nasibu-diamond-platnumz-243-rickmedia

Staa wa Muziki #Zuchu anaua uvumi wa kuwa Aliolewa Na #Diamond Na kisha kupewa Talaka 3, Kupitia Bio yake ya Instagram Ameongeza utambulisho wa kuwa yeye ni #MrsDiamondPlatnumz.

Siku kadhaa zilizopita Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Aliandika Ujumbe huu kuhusu Ndoa yake na #Zuchu

Miongoni Mwa vitu ambavyo nimejifunza ni Ukomavu wa Kukaa kimya… Ukomavu huu unataka uvumilivu wa hali ya juu, Inataka uwe na moyo wa Subra na hasa kukaza roho pindi mtu au watu wanapokua wanakupakazia ubaya fulani kwenye jamii halaf wewe una Ukweli wake lakini unatakiwa ukae tu kimya Usijibu ilhali ukweli unao ndani…Kwakweli si jambo jepesi linataka Ustahmilivu wa hali ya juu sana, na siwezi sema eti nauweza sana, lakini namshukuru Mwenyez Mungu amenijaalia Hekima hio kwa kiwango chake, na Nimekua nikiishi hivyo kwa Muda mrefu kukaa kimya pindi yoyote akijaribu kusema lolote zidi yangu, na ndio maana ata interview nimekua naepuka kufanya skuizi… japo si jambo jepesi lakini faida yake nimeiona na ni kubwa maana vita vyako inakua unapambaniwa na Mwenyez Mungu na inakufanya Uwe Mshindi kila siku….Anyways: Najua kila mmoja wenu ana picha tofauti kabisa kuhusu Diamond Platnumz na KUOA, ila tu nataka leo niwaambie kuwa HUYU DIAMOND PLATNUMZ ALISHAWAHI KUOA , na kuna siku nitawaambia ikawaje.