#EthanCrumbley, kijana aliyeua wanafunzi 4 wakati wa shambulio la risasi katika shule ya #Michiganhighschool amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa kuachiliwa.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alipewa hukumu yake Ijumaa utakumbuka, #Crumbley aliwaua wanafunzi wenzake 4 na kuwajeruhi watu wengine 7 alipofyatua risasi katika Shule ya #Michiganhighschool ya Oxford, katika kitongoji cha Detriot cha Oxford Township, MI.
#Crumbley aliiambia mahakama kwamba alikuwa mtu mbaya sana kabla ya kuhukumiwa kifungo chake kikubwa na kuongeza kuwa amekuwa akijaribu kufanya vizuri zaidi katika maisha yake lakini anakiri anakiri amefanya mambo ya kutisha ambayo hakuna mtu anayepaswa kufanya.