Mmarekani mwenye umri wa miaka 44 aliyetembelea #Bahamas kutoka #Boston aliuawa katika shambulio la papa alipokuwa akipanda kasia karibu na eneo la mapumziko la ufuo siku ya Jumatatu, kulingana na mamlaka ya eneo hilo.
Mwanamke huyo ambae inadaiwa alisafiri na kwenda Bahamas akiwa na Mwanaume mmoja kwa ajili ya mapumziko alishambuliwa na papa baada kuvamia kasia waliyokuwa wamepanda.
Mlinzi katika kituo hicho cha mapumziko aliona shambulio hilo na akaingia majini kwa boti kujaribu kuokoa mwathiriwa pamoja na jamaa lakini hakufaikiwa kuokoa maisha ya Mwanamke huyo.