Uzembe wa watoa Huduma za Afya wasababisha kifo cha mjamzito Tanga

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 months ago
rickmedia: uzembe-watoa-huduma-afya-wasababisha-kifo-cha-mjamzito-tanga-859-rickmedia

Tume iliyoundwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kuchunguza kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro aliyefariki Novemba 11, 2023 imesema sababu za Kifo chake ni uzembe wa Wataalamu wa Afya na sio kukosa Tsh. 150,000

Akizungumza kuhusu uchunguzi, Mwenyekiti wa Tume, Dkt. Ali Said amesema Wataalamu hawakuchukua hatua za haraka wakati Mjamzito akiwa katika hali ya hatari. Pia, walimcheleweshea Upasuaji na Daktari hakutoa Rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya

Baada ya kupokea Ripoti hiyo, Waziri Ummy amesema tayari Baraza la Madaktari pamoja na Wauguzi na Wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa Wataalamu wawili wa Afya waliohusika na tukio hilo