Ifikapo saa 4 Asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki Bunge la Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania linatarajiwa kuanza na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia na kufungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 14, 2025.
Mbali na hotuba ya Rais Samia kusubiriwa kwa hamu na wananchi mbalimbali, pia Rais Samia atamuapisha Waziri Mkuu Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye siku ya jana Waheshimiwa Wabunge walimthibitisha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura 369 baada ya Rais Samia kupendekeza jina lake.
Wewe unaisubiri hotuba ya Rais Samia ukiwa wapi?