Rais Mstaafu wa Brazil 'Jair Bolsonaro' Ahukumiwa kifungo cha zaidi ya Miaka 27 Jela

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

15 hours ago
rickmedia: rais-mstaafu-brazil-jair-bolsonaro-ahukumiwa-kifungo-cha-zaidi-miaka-jela-640-rickmedia

Rais Mstaafu wa Brazil, Jair Bolsonaro amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kubadili matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2022 ili aendelee kubaki madarakani.

Bolsonaro ametiwa hatiani kwa makosa matano ikiwemo kupanga mapinduzi ya kijeshi na kujaribu kumuua Rais Mteule (wakati huo), Luiz Inácio Lula da Silva.