Msanii #ChidiBenz amesema amewahi kupata mafanikio makubwa kuliko wasanii wengi wa sasa, akisisitiza kuwa wakati wake hakuna aliyemzidi isipokuwa Lucas Mkenda (Mr Nice).
Amedai baada ya #MrNice kuibuka, nafasi yake ilifuata na akafanikiwa sana licha ya kutoka mtaani Ilala.
#ChidiBenz pia amekiri alikuwa akitembea na watu wengi, jambo ambalo hata Joseph Kusaga aliwahi kumwonya.
Mbali na hivyo #ChidiBenz amesema kuwa watu wasimhukumu kwa ulevi aliopitia kwani amefanya muziki kwa zaidi ya miaka 22 na hata kushiriki kampeni za marais watatu.
Amesema changamoto za maisha ndizo zilimpeleka kwenye pombe na dawa za kulevya, lakini anashukuru msaada aliopata na sasa anasisitiza kwamba suluhisho la kweli ni yeye mwenyewe kusimama na kuacha matumizi ya dawa hizo.
amefunguka kuhusu maisha ndani ya sober house akisema ni magumu zaidi kuliko jela.
Amesema hukaa muda mwingi bila kufanya shughuli yoyote zaidi ya kula na kulala, hali iliyomfanya kunenepa kutokana na kula vyakula vya kawaida kama chips na kuku.
"Nimeingia sober House nyingi ila hii... Unajua kulala na kuamka na kula na kuamka bora jela. Kule jela mnatembea lakini kule sober makaa na kula na kunywa.
Nakuwa nawaza sana vitu vingi kwahiyo nalala sana. Ndio maana nimenenepa hivi. Nilikuwa nakula chakula hicho hicho kama chips, kuku. Nalala sifanyi chochote"