Bunge la mpito la Burkina Faso limepitisha sheria inayopiga marufuku ushoga, ambapo wahusika wanaweza kufungwa hadi miaka mitano. Sheria hiyo mpya, inayojulikana kama Persons and Family Code, Sheria hii inawahusu watu wenye uraia na watu wasio na uraia.
Sheria hii imepitishwa na bunge lisilochaguliwa lenye wanachama 71, na sasa inasubiri kutiwa saini na kiongozi wa kijeshi, Ibrahim Traoré. Waziri wa Sheria, Edasso Rodrigue Bayala, alisema kuwa sheria inaanza kutumika mara moja, na watu watakaorudia kosa hilo na si raia wa nchi hiyo watafukuzwa.
Burkina Faso inajiunga na nchi nyingine za Afrika kama Uganda na Senegal ambazo zimeweka sheria kali dhidi ya LGBTQ+, huku mataifa kama Afrika Kusini, Botswana na Angola yakiwa yamehalalisha au kulinda haki za watu wa LGBTQ+.
Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso, iliyochukua mamlaka kwa mapinduzi mwaka 2022, imekuwa ikizidi kukandamiza upinzani wakati mapigano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu yakiendelea.