Mahakama ya Hakimu Mkazi huko Ikorodu imeamuru vipimo viwili vya DNA kufanywa kwa Liam Aloba, mwana wa marehemu msanii wa Nigeria, Ilerioluwa Aloba almaarufu Mohbad.
Agizo hilo lilitolewa Septemba 2, 2025, kufuatia ombi la baba wa Mohbad, Joseph Aloba, aliyekuwa akitaka uthibitisho wa uzazi.
Mahakama ilikubali vipimo vifanyike Nigeria na pia nje ya nchi kwa gharama ya mwombaji, huku pande zote zikihusishwa katika uchukuaji wa sampuli. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 11, 2025.
Mohbad alifariki Septemba 12, 2023, baada ya kuumia mkononi na kupata kifafa ghafla. Alizikwa siku iliyofuata, lakini mwili wake ulifukuliwa tena kwa agizo la serikali kwa ajili ya uchunguzi wa kina. Ripoti ya awali ya uchunguzi haikuweza kubaini chanzo cha kifo kutokana na kuoza kwa viungo vya ndani.