Rais Wa Zamani wa Peru Afungwa Jela kisa Ufisadi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

20 hours ago
rickmedia: rais-zamani-peru-afungwa-jela-kisa-ufisadi-157-rickmedia

Rais wa zamani wa Peru, Alejandro Toledo (78), amehukumiwa kifungo cha miaka 13 na miezi 4 jela kwa makosa ya utakatishaji fedha alipokuwa madarakani (2001–2006). 

Inadaiwa alitumia fedha za rushwa kutoka kampuni ya ujenzi ya Brazil, Odebrecht (sasa Nononor), kununua mali zenye thamani ya dola milioni 5.1 kupitia kampuni ya Costa Rica aliyoianzisha kwa ajili ya kuficha fedha hizo.

Hii ni hukumu yake ya pili, kwani Oktoba 2024 alishahukumiwa kifungo cha miaka 20 na miezi 6 kwa kupokea rushwa kutoka Odebrecht ili kuipa kampuni hiyo zabuni za miradi mikubwa.

Toledo amekana mashtaka na kudai Serikali imepanga njama dhidi yake. 

Hukumu hii inamuweka kwenye orodha ya marais wa zamani wa Peru waliowahi kufungwa kwa tuhuma za ufisadi, akiwemo Ollanta Humala, Pedro Castillo na Martin Vizcarra, ambao pia wamewahi kushikiliwa katika kituo maalumu cha viongozi wa zamani.