Marekani Yashambulia Meli Iliyokuwa Ikisafirisha Madawa Ya Kulevya

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: marekani-yashambulia-meli-iliyokuwa-ikisafirisha-madawa-kulevya-526-rickmedia

Rais Donald Trump ametangaza kuwa Marekani imeishambulia meli ya kusafirisha dawa za kulevya kusini mwa Karibea na kuwaua wanachama 11 wa genge la Venezuela Tren de Aragua. 

Trump alisema meli hiyo ilikuwa kwenye maji ya kimataifa ikielekea Marekani. 

Hatua hii imekuja wakati utawala wake unaongeza shinikizo la kijeshi na kisiasa dhidi ya Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, ikiwemo zawadi ya dola milioni 50 kwa atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati.