Ahukumiwa Miaka 6 kwa makosa ya Kigaidi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: ahukumiwa-miaka-kwa-makosa-kigaidi-475-rickmedia

Mahakama ya Wilaya ya Päijät-Häme, Finland, imemhukumu #SimonEkpa kifungo cha miaka 6 jela kwa makosa ya ugaidi. 

#Ekpa, mkazi wa Lahti na mwanasiasa wa zamani wa eneo hilo, alipatikana na hatia ya Kuchochea ugaidi na kushiriki katika shughuli za kundi la kigaidi kupitia ushawishi wake mkubwa wa mitandao ya kijamii, Kusambaza silaha, mabomu na risasi kwa baadhi ya makundi nchini Nigeria, Kuwahimiza wafuasi wake kufanya uhalifu kusini mashariki mwa Nigeria, Pia alitiwa hatiani kwa udanganyifu mkubwa wa kodi na kukiuka sheria ya mawakili.

Ekpa alikanusha mashitaka yote, lakini mahakama ilisema makosa hayo yalifanywa akiwa Finland hivyo ikawa na mamlaka ya kutoa hukumu.