Rais wa Indonesia, Prabowo Subianto, ametangaza kupunguza mishahara na marupurupu ya wanasiasa, ikiwemo wabunge, kufuatia maandamano makubwa yaliyosababisha vifo na uharibifu wa miundombinu Nchini humo.
Maandamano hayo yamechochewa na kupanda kwa posho za wabunge na kifo cha dereva aliyepigwa na askari. Aidha, Rais ameahirisha safari yake ya China na kuonya kuwa maandamano yasipodhibitiwa yanaweza kugeuka uhaini na ugaidi.