Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo, Juma Duni Haji, ameiomba Halmashauri Kuu ya Chama chake isijadili na kupitisha jina lake katika kinyang’anyiro cha kuusaka Uenyekiti wa Chama, akisema anamuunga mkono Othman Masoud Othman anayewania nafasi hiyo.
Haji Duni ametangaza uamuzi huo leo Machi 4, 2024, Siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo utakaowachagua Viongozi wakuu wa Kitaifa. Awali alilalamika kuhujumiwa kuelekea Mchakato huo.