Rapa wa Marekani, J. Cole, amezua mjadala kwa mashabiki wake baada ya kuonyesha ishara zinazoweza kuashiria kustaafu muziki. Wengi walivutiwa na picha aliyovaa ya hoodie yenye maandishi ya “I’m Retired,” jambo lililosababisha uvumi mtandaoni.
Hata hivyo, J. Cole hajatangaza rasmi kustaafu, badala yake ametangaza album yake mpya, “The Fall‑Off,” itakayoachiwa Februari 6, 2026, ambayo baadhi ya mashabiki wanafananisha jina lake kama ishara ya uwezekano wa kustaafu.
Rapa huyo amekuwa akieleza kakwenye mahojiano kwamba anaweza kuacha muziki siku moja, lakini hajatoa muda kamili au tangazo la mwisho. Kwa sasa, mashabiki wanangojea kuona iwapo The Fall‑Off itakuwa mwisho wa safari yake ya muziki au ni mwanzo wa sura mpya.