Binti anayejitambulisha kama Anu Adeleke Amemuomba hadharani nyota wa muziki wa Nigeria Davido afanyiwe kipimo cha DNA kuthibitisha uhusiano wao.
Anu anasema amekumbana na ubaguzi na changamoto za kisaikolojia tangu utotoni kutokana na madai hayo, ingawa amefaulu masomoni na kuendelea kujijenga.
Akiwa anaelekea utu uzima, amesema anatafuta ukweli na amani ya moyo, akisisitiza ombi lake ni la heshima na binafsi. Ujumbe wake umeibua mjadala mkubwa mitandaoni.
.