Xabi Alonso ajiuzulu nafasi yake ya Meneja Klabu ya Real Madrid baada ya Miezi 7

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

18 hours ago
rickmedia: xabi-alonso-ajiuzulu-nafasi-yake-meneja-klabu-real-madrid-baada-miezi-609-rickmedia

Real Madrid Jumatatu, Januari 12, 2026 imetangaza kuwa meneja wake Xabi Alonso amejiuzulu wadhifa wake kwa makubaliano binafsi.

Xabi Alonso ameondoka Real Madrid baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miezi saba kama meneja.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu hiyo ameondoka kwa makubaliano ya pande zote kufuatia kipigo cha mabao 3-2 ambacho imekipata kutoka kwa Barcelona katika fainali ya Kombe la Supercopa jana Jumapili, huku timu yake ikiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya klabu hiyo Barcelona iliyo kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.

Nafasi ya Alonso itakaimiwa na nyota wa zamani wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa ambaye anafundisha kikosi cha vijana cha klabu hiyo.