Wenyeji wa michuano ya AFCON 2025, Morocco imekuwa timu ya pili kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Cameroon mabao 2-0.
Mshambuliaji wa Morocco, Brahim Diaz ameendelea kufukuzia ufungaji bora akiifungia timu yake bao la kwanza na kufikisha mabao matano huku bao la pili la mchezo likifungwa na Ismael Saibari.
Morocco itavaana na Senegal katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Januari 14, 2026.