Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Marekani inaweza kufanya mashambulizi zaidi ya anga nchini Nigeria iwapo mauaji ya Wakristo yataendelea.
Katika mahojiano na New York Times, Trump alisema angependa mashambulizi ya hivi karibuni yawe ya mara moja, lakini akaongeza kuwa yatarejea endapo ghasia dhidi ya Wakristo hazitakoma.
Awali, utawala wake ulikosoa serikali ya Nigeria kwa kushindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya mashambulizi ya wanamgambo wenye itikadi kali.