Jaji aamuru mali za Young Thug zilizokuwa zimekamatwa rudishwe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: jaji-aamuru-mali-young-thug-zilizokuwa-zimekamatwa-rudishwe-556-rickmedia

Jaji aliyekuwa Akiendesha Kesi ya Rapa Young Thug ‘Paige Reese Whitaker’ Ameziamuru Mamlaka Zirudishe Mali Za Rapa Huyo zilizokuwa zimekamatwa.

Mamlaka zilikuwa zimechukua magari ya kifahari, vito vya thamani na kiasi cha dola 150,000 (takribani TSh milioni 390) wakati wa uchunguzi wa kesi dhidi ya lebo yake ya YSL ( Young Stoner Life Records). Hata hivyo, baada ya kesi ya kutaifishwa mali (civil forfeiture) kufutwa Agosti 18, 2025, mali hizo sasa zitarudishwa kwa msanii huyo.

Young Stoner Life Records ni label iliyoanzishwa na Young Thug na imewahi kusajili wasanii wakubwa kama Gunna na Lil Keed. Hata hivyo, waendesha mashtaka walidai YSL ni genge la uhalifu madai ambayo Young Thug na wenzake walikanusha wakisisitiza kuwa ni label ya muziki pekee.