Wakamatwa kwa tuhuma za uporaji wakiwa na jeneza

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: wakamatwa-kwa-tuhuma-uporaji-wakiwa-jeneza-318-rickmedia

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu wanne kwa tuhuma za unyang’anyi, uporaji na kuwajeruhi wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji. Tukio hilo lilitokea Januari 8, 2026 saa 8:40 mchana, Mabwepande wilayani Kinondoni.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro, amesema kundi la watu waliokuwa wamepanda pikipiki na wengine wakiwa na silaha za jadi, walifanya vitendo hivyo wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Ibrahimu Elia.

Marehemu anadaiwa kuuawa Januari 2, 2026 Bunju baada ya kutuhumiwa kujihusisha na uporaji wa pikipiki, na baadaye kuzikwa na ndugu zake Mabwepande.