Wizkid awa msanii wa kwanza Afrika kufikisha wasikilizaji Bilioni moja Spotify

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: wizkid-awa-msanii-kwanza-afrika-kufikisha-wasikilizaji-bilioni-moja-spotify-724-rickmedia

Staa wa Afrobeats kutoka Nigeria, Wizkid, ameandika historia baada ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kufikisha streams bilioni 10 kwenye Spotify. Hii ni pamoja na nyimbo zake binafsi, kolabo, na ushiriki wake kwenye nyimbo za wasanii wengine.

Kila stream huhesabiwa pale wimbo unapochezwa kwa angalau sekunde 30, na namba hizi zinathibitisha kwa nguvu kwamba muziki wa Wizkid unasikilizwa duniani kote. Mafanikio haya sio tu ya Wizkid pekee, bali ni ushindi mkubwa kwa muziki wa Afrika, ikiashiria ukuaji wa Afrobeats na ushawishi wake kwenye masoko makubwa ya kimataifa.

Hii rekodi pia ina maana kubwa kibiashara, inafungua milango kwa mikataba ya kimataifa, inapanua ushawishi wa Wizkid, na inatoa nafasi kwa wasanii wengine wa Kiafrika kufuata nyayo zake. Kwa mashabiki wa muziki, namba hizi ni uthibitisho halisi wa nguvu ya Afrobeats na nafasi ya Afrika kwenye ramani ya muziki wa dunia.