Ajali ya Basi yaua watu wanne Korongwe Jijini Dar Es Saalam

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

12 hours ago
rickmedia: ajali-basi-yaua-watu-wanne-korongwe-jijini-dar-saalam-349-rickmedia

Watu wanne wamepoteza maisha kufuatia magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Mkumbara, Tarafa ya Mombo, wilayani Korogwe, kwenye barabara kuu ya Same–Korogwe.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Alimachius Mchunguzi, imeeleza ajali hiyo ilitokea saa 9:30 usiku wa kuamkia leo, ikihusisha lori la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T 812 ELQ, lililokuwa limeunganishwa na tela lenye namba T 106 DGS, mali ya kampuni ya Mikoani Edible Oil and Detergents Ltd, likitokea Same kuelekea Korogwe.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa lori hilo iligongana uso kwa uso na basi aina ya Yutong lenye namba ya usajili T 579 ECH, mali ya kampuni ya Mwensino, lililokuwa likitokea wilayani Lushoto kuelekea mkoani Arusha.

Amesema katika ajali hiyo, watu wanne walifariki na 16 wamejeruhiwa, wakiwemo madereva wa vyombo hivyo na wote walikimbizwa Kituo cha Afya Mombo kwa matibabu,