Memba wa Wu-Tang Clan, RZA, amezungumzia jinsi teknolojia ya AI inavyoweza kuokoa muda na gharama za pesa kwenye utayarishaji wa muziki. Kupitia jukwaa la “From Concept to Reality: Creatives Using AI to Bring Big Ideas to Life” la Consumer Electronics Showcase, RZA alisema:
"Ubunifu ni muda. Kazi ambayo ingechukua siku tatu kupata matokeo mazuri, na kutumia msaidizi wa AI inaweza kufanyika kwa saa tatu tu."
RZA alielezea jinsi alivyotumia AI kuunda demo ya albamu yake ya 2024 ya muziki wa classical, A Ballet Through Mud. Badala ya kutumia siku 10-12 kufanikisha rekodi ya orchestra, AI ilimrahisishia kufanya kazi hiyo ndani ya siku moja, huku akiepuka gharama kubwa za kuajiri orchestra, ambazo zingefikia hadi dola 60,000 kwa siku.
RZA pia alisema kuwa Google Gemini ndio jukwaa lake anayependelea zaidi kutumia. Hata hivyo, matumizi ya AI katika hip-hop yameibua maoni mchanganyiko. Wakati baadhi ya wasanii wakiutumia, wengine wamesema hawakubali.
Baadhi ya mashabiki mtandaoni walihisi hatua hii ni ya kuvunja moyo, huku wengine wakiona kama maendeleo ya lazima kwa wasanii wa kizazi cha sasa.