Upinzani Togo waitisha maandamano kupinga Ucheleweshwaji wa Uchaguzi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

9 months ago
rickmedia: upinzani-togo-waitisha-maandamano-kupinga-ucheleweshwaji-uchaguzi-417-rickmedia

Vyama Vinne vya Upinzani vimeitisha Maandamano makubwa kuanzia Aprili 8, 2024 ili kupinga kucheleweshwa kwa Uchaguzi Mkuu uliotarajiwa kufanyika Aprili 20, 2024 huku tarehe mpya ikiwa bado haijawekwa wazi.

Vuguvugu la Kisiasa limeongezeka Nchini humo baada ya Bunge kupitisha mabadiliko ya Katiba ambapo Vyama vya Upinzani vimelaani hatua hiyo vikidai inaweza kumruhusu Rais Faure Gnassingbé kusalia Madarakani.

Rais Gnassingbé amekuwa Madarakani tangu Mwaka 2005, alipomrithi Baba yake ambaye aliongoza Togo kwa Miaka 38.