Korea Kaskazini yafanya jaribio la kurusha Kombora la masafa ya kati

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 week ago
rickmedia: korea-kaskazini-yafanya-jaribio-kurusha-kombora-masafa-kati-468-rickmedia

Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa ya kati ikiwa ni mwendelezo wa majaribio yake ya silaha.

Kombora hilo limerushwa wakati ambao Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken anaendelea na ziara yake nchini Korea Kusini.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu Januari 6, 2025 na Jeshi la Korea Kusini ilisema kombora hilo lilielekezwa upande wa Mashariki ya Korea Kaskazini muda mfupi baada Blinken kuanza mazungumzo na Rais wa Mpito wa Korea Kusini, Choi Sang-mok.

“Jeshi letu lilinasa taarifa ya kurushwa kwa kombora la masafa ya kati kutoka nchini Korea Kaskazini,” ilisema taarifa ya Jeshi hilo na kuripotiwa na tovuti ya Al Jazeera.

Taarifa ya Jeshi la Korea Kusini pia imesema kombora hilo la majaribio, linaelezwa kwenda umbali wa Kilometa 1,100 (maili 680), kabla ya kutua ardhini na kupiga baharini eneo la Peninsula ya Korea na Japan huku ikidokeza kuwa ufuatiliaji wa kina unaendelea.