Balozi Dkt Wilbroad Slaa amekwama kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Januari 10, 2025 baada ya Upande wa Jamhuri kuwasilisha kiapo cha kupinga Dkt. Slaa asipewe dhamana kwa sababu ya Usalama wake
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Wakili Boniface Mwakubusu amesema kosa analotuhumiwa nalo Dkt. Slaa ni kosa ambalo lina dhamana na pia wanaohofiwa kumshambulia ndio wangekamatwa ili aweze kupewa dhamana na kuwa salama
Aidha, upande wa Jamhuri umesema upelelezi haujakamilika na hivyo, Mahakama imeahirisha shauri hilo hadi Januari 13, 2025.