Msanii wa #RocNation, #VictoryBoyd, amefungua kesi dhidi ya #TravisScott, #Future, na #SZA, akiwatuhumu kwa ku-copy vipengele muhimu kutoka kwenye wimbo wake wa 2019, “Like The Way It Sounds,” kwenye wimbo wao “Telekinesis.”
Wimbo huo, uliozinduliwa mwaka 2023, ulikaa kwenye chati ya Hot 100 kwa wiki 11. #Boyd anadai kuwa awali aliushirikisha wimbo wake kwa #KanyeWest, ambaye aliurekodi kama “Ultrasounds” kabla ya kudaiwa kuupitisha kwa #Scott. Kutoka hapo, anadai kuwa #Scott alishirikisha wimbo huo kwa #Future na #SZA, ambao waliongeza michango yao kwenye “Telekinesis.”
Kesi hiyo pia inamtaja mtengenezaji wa saa za kifahari, Audemars Piguet, ambaye alishirikiana na Cactus Jack ya Scott kwa laini ya saa zilizotangazwa kwa kutumia “Telekinesis.” Boyd anasema hakuwahi kuidhinisha kazi yake itumike katika kampeni hiyo.
Mpaka sasa, hakuna yeyote kati ya walalamikiwa aliyetoa taarifa rasmi kuhusu madai hayo, na pia hakuna ripoti za majibu rasmi.