Washauri 3 wa Rais wa Burundi Ndayishimiye wafungwa kwa uhaini

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

12 hours ago
rickmedia: washauri-rais-burundi-ndayishimiye-wafungwa-kwa-uhaini-441-rickmedia

Washiriki watatu waandamizi wa timu ya ushauri ya Rais Evariste Ndayishimiye wamepelekwa Gereza Kuu la Mpimba, #Bujumbura, wakikabiliwa na tuhuma za Uhaini.

Maafisa hao wanatuhumiwa kuwaachia huru baadhi ya Wafungwa wa Makosa ya Ubakaji na Mauaji ambao hawakuwemo kwenye Orodha ya Wafungwa waliopata Msamaha wa Rais.