Kampuni ya kutengeneza vifaa mbalimbali vya mawasiliano Apple, imeripotiwa kuwa na mpango wa simu zake zijazo za ‘Iphone’ kuanza kutumia kamera za Samsung.
Imeelezwa kuwa Samsung itaanza kutengeneza sensor mpya yenye uwezo zaidi huku Apple ikitemana na Exmor RS kutoka kampuni ya Sony ambayo ndio hutumika kwenye simu zao za sasa.
Sensor hiyo mpya italeta mabadiliko zaidi kwenye upande wa kamera za Iphone kwa kuongeza uwezo wa kukusanya mwanga na kuifanya kamera kuwa nyepesi wakati wa kutumia.
Simu ambazo zitaanza kutumia Sensor hiyo mpya ni toleo la Iphone 18 ambayo huenda ikatoka mwaka 2026. Mbali na kampuni hiyo kutaka kutumia kamera za Samsung lakini pia baadhi ya simu zake zimekuwa zikitumia chaji za USC-C kama za Samsung.