Taarifa ya Mmiliki wa META, Mark Zuckerberg imesema majaribio ya utaratibu wa kutumia Madokezo ya Kijamii (Community Notes) kuhakiki Maudhui utaanza kwa Watumiaji waliopo Marekani na baadaye utaendelea kwa watumiaji Duniani kote.
Awali, META ilikuwa ikitumia timu maalumu ya Uhakiki wa Maudhui na Mifumo ya Kiotomatiki, utaratibu ambao ulikuwa ukilalamikiwa kuwa unabana Uhuru wa Kujieleza
Inadaiwa kuwa hatua hiyo ni mkakati wa META kujenga uhusiano na Utawala mpya wa Rais Donald Trump atakayeingia Ikulu Januari 20, 2025.