Rais wa Ukraine #Zelenskyy ameonesha Nia ya kutuma Msaada wa Wazima moto 150 kwenda Marekani kwa ajili ya kusiaidia kuokoa Maisha katika moto wa California.
“Leo, niliagiza Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine na wanadiplomasia wetu kujiandaa kwa uwezekano wa kushiriki waokoaji wetu katika kukabiliana na moto wa msituni huko California.
Hali huko ni ngumu sana, na Waukraine wanaweza kusaidia Wamarekani kuokoa maisha.
Hivi sasa, tunaendelea kuratibu, na tumetoa msaada wetu kwa upande wa Marekani kupitia njia husika. Waokoaji wetu 150 tayari wako tayari”.
Watabiri wa hali ya hewa huko California wemesema kuwa upepo mkali ambao ulisababisha moto Los Angeles unatarajiwa kushika kasi tena wiki hii, huku vikosi vya zima moto vikiendelea kudhibiti moto huo.
Takriban watu 24 wamefariki katika moto huo huku moto mingine mikubwa miwili ikiendelea kuwaka katika mji mkubwa wa California.