Mwanamuziki #MeganTheeStallion ameshinda shauri la kizuizi dhidi ya #ToryLanez baada ya kutoa ushahidi kwa machozi mbele ya jaji wa Los Angeles akieleza kuwa anaogopa #Tory atakaporuhusiwa kutoka gerezani, anaweza kumpiga risasi tena na labda safari hii kuna uwezekano wa kupoteza maisha.
Mwezi mmoja baada ya mawakili wa nyota huyo kuonya kwamba #Lanez ameendelea na kampeni ya unyanyasaji hata akiwa gerezani, Jaji Richard Bloom alitoa agizo la kizuizi cha kiraia ambalo litamzuia #Lanez kufanya vitendo vyovyote vya unyanyasaji kwa miaka mitano ijayo.
Jaji Bloom alitoa agizo hilo mahakamani, akisema kwamba Megan ameonyesha tishio halisi la vurugu na vitendo vingine vya uwezekano wa unyanyasaji ambavyo vinamtatiza mlalamikaji.
Tory Lanez amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kumpiga risasi Megan Thee Stallion miguuni. Mahakama nchini Marekani ilimpata na hatia ya kumpiga risasi mwimbaji Savage huko Hollywood Hills wakati wa mabishano.